FRANKFURT: Merkel amefungua maonyesho ya magari | Habari za Ulimwengu | DW | 13.09.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

FRANKFURT: Merkel amefungua maonyesho ya magari

Kansela wa Ujerumani,Angela Merkel amefungua rasmi maonyesho ya 62 ya magari mjini Frankfurt. Kiini cha maonyesho ya mwaka huu ni ulinzi wa mazingira.

Viwanda vya magari vimeania kuonyesha kuwa vinaunga mkono juhudi za kupambana na tatizo la ongezeko la ujoto duniani.Kansela Merkel amesema,viwanda vya magari lazima vifikirie njia za kupunguza uzalishaji wa gesi ya kaboni dayoksaidi.

Zaidi ya mashirika 1,000 yanayohusika na magari yanawakilisha nchi 40 katika maonyesho ya siku kumi mjini Frankfurt.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com