FRANKFURT AM MAIN: Klein amerejea Ujerumani baada ya kuwa jela Iran | Habari za Ulimwengu | DW | 14.03.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

FRANKFURT AM MAIN: Klein amerejea Ujerumani baada ya kuwa jela Iran

Mjerumani Donald Klein amerejea Ujerumani baada ya kuwa jela kwa takriban miezi 16 nchini Iran. Kwa mujibu wa polisi,Klein alie na umri wa miaka 53 aliwasili uwanja wa ndege wa Frankfurt-am-Main ambako alipokewa na familia yake.Klein alikamatwa Novemba mwaka 2005,baada ya kuingia katika bahari ya Iran akiwa katika mashua ya tanga.Baada ya kufikishwa mahakamani,Klein alipewa kifungo cha jela cha mwaka mmoja na nusu hapo Januari 2006.Aliachiliwa huru siku ya Jumatatu mjini Teheran.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com