1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Frank-Walter Steinmeier atagombea kiti cha Kansela wa Ujerumani mwakani

Nijimbere, Gregoire7 Septemba 2008

Frank- Walter Steinmeier, ameteuliwa na chama cha Socio-demokrate cha SPD kuwa mgombea wa kiti cha Kansela wa Ujerumani mwakani. Steinmeier atashindana na Kansela Angela Merkel, kutoka chama cha Konsevative cha CDU.

https://p.dw.com/p/FD56
Frank-Walter SteinmeierPicha: AP

Maafisa wakuu wa chama cha SPD wamechukuwa hatua hiyo muda mfupi tu uliyopita katika mkutano unaoendelea huko Werder nje ya mji mkuu wa Ujerumani wa Berlin. Katika mkutano huo pia mwenyekiti wa chama cha SPD, Kurt Beck, amejiuzulu. Udadisi wa maoni ya raia uliyonyesha kuwa umarufu wa Kurt Beck ulikuwa umepungua mno mnamo siku za nyuma.


Frank-Walter Steinmeier ambae ni waziri wa mambo ya kigeni, ndiye pia ataongoza kwa muda chama cha SPD hadi uteuzi wa kiongozi mpya wa chama haraka iwezekanavyo. Inaaminiwa mwenyekiti huyo mpya wa chama cha SPD atakuwa, Franz Müntefering, mwenye umri wa miaka 68 na kiongozi wa zamani wa chama hicho cha SPD na ambae amerejea kwenye uwanja wa kisiasa baada ya kusitisha kwa muda shughuli za kisiasa.


Kulingana na katibu mkuu wa chama cha SPD, Hubertus Heil, uongozi wa chama ndiwo utapanga tarehe ya mkutano mkuu wa chama ambapo atateuliwa mwenyekiti mpya wa chama.