1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

February 13-kumbu kumbu za siku Dresden iliposhambuliwa

Madege yanchi shirika zilizopigana vita dhidi ya Ujerumani ya wanazi yaliuteketeza mji wa Dresden muda mfupi kabla ya vita vikuu vya pili kumalizika mwaka 1945.

A child lights candles commemorating the 67th anniversary of the Allied bombing of Dresden during WWII in Dresden, Germany, Monday, Feb. 13, 2012. British and U.S. bombers on Feb. 13-14, 1945 destroyed Dresden's centuries-old baroque city center. (Foto:Jens Meyer/AP/dapd)

Dresden yakumbuka mashambulio ya mabomu ya februuary 13 mwaka 1945

Ilikuwa saa nne na kitu hivi ,februari 13 mwaka 1945 pale ndege chungu nzima za kivita nyingi zikiwa mpya kutoka Uingereza zilipolivamia anga ambalo halikuwa na hata kiwingu la Dresden.Ndege hizo zlihitaji dakika 15 tu,kuigeuza magofu na majivu robo tatu ya eneo la kati la mji huo.Saa chache baadae likafuata wimbi la pili la mashambulio lililozusha dharuba ya moto.Miezi mitatu baadae kile kilichokuwa kikijulikana kama " enzi ya tatu" ikasalim amri bila ya masharti.

Kengele za Makanisa zinalia

Ili kukumbuka mashambulio hayo ya mabomu,tangu mwaka 1946,kila Februari 13 kengele hupigwa katika makanisa ya Dresden.Lakini tangu mwaka 1998 kivuli cha kiza kimetanda juu ya kumbukumbu hizo.Wafuasi wa siasa kali ya mrengo wa kulia wanazitumia kumbu kumbu hizo ili kukanusha makosa ya Ujerumani katika vita na pia mauwaji ya halaiki ya wayahudi Holocaust.Kile kilichoanzia kwa kukusanyika watu chini ya mia moja,kimekujageuka kuwa mkutano wa hadhara wa umati.Hadi wanazi mambo leo 6500 wamekuwa wakishiriki mnamo miaka ya nyuma katika kile wanachokiita "Maandamano ya msiba"katika eneo la kati la Dresden.

Ili kulivunja nguvu jinamizi wakaazi wa Dresden na wengine wa maeneo mbali mbali wamekuwa na wao pia wakiandamana kulaani kuchipuka upya siasa kali za mrengo wa kulia.Karibu watu 15 elfu walishiriki mwaka 2011 katika maandamano ya watu waliokamatana mikono mfano wa myonyoro.Ushirika wa "Dresden bila ya wanazi" ukaanzisha kampeni ya kufunga njia"kuzuwia maandamano ya wanazi mambo leo.Mapigano makali yakaripuka pamoja na polisi waliowaandama kwa nguvu wanaharakati waliokuwa wakiandamana dhidi ya wanazi .Kwa mtazamo wa serikali ya jimbo kampeni ya kufunga njia haiambatani na ruhusa iliyotolewa ya watu kuandamana.

Sachsen/ Ein Teilnehmer eines Neonazi-Aufmarschs am 67. Jahrestag des alliierten Bombenangriffs auf Dresden vom 13. Februar 1945 haelt am Montag (13.02.12) in Dresden kurz vor Beginn eine Fahne. Bei dem Aufmarsch wurden bis zu 2.000 Rechtsextreme erwartet. Seit Jahren missbrauchen Rechtsextreme das Gedenken an die Opfer der Bombardements fuer ihre Zwecke. (zu dapd-Text) Foto: Jens Schlueter/dapd

Polisi wazuwia machafuko wakati wa maandamano ya wanazi mambo leo

Baraza kuu la Wayahudi linaunga mkono kampeni hiyo.

Kama ilivyokuja bainika baadae,vikosi vya usalama vilikusanya data za wanaharakati zaidi ya milioni moja kutoka simu za mkono.Walihusika pia wale waliokuwa wakiandamana kwa amani na hata wakaati ambao hawaakushiriki katika kampeni hiyo.Wanasiasa na maafisa wa serikali katika jimbo la Sachsen tangu wakati huo wamekuwa wakikabwa na lawama za kuwaandama wapinzani wa wanazi mambo leo.Katibu mkuu wa baraza kuu la wayahudi nchini Ujerumani Stephan Kramer anazungumzia juu ya "kubadilisha hali ya mambo na madowa."Ameunga mkono kinaga ubaga kampeni ya wanaowapinza wanazi mambo leo.Kwa mujibu nwa "Ushirika wa Dresden bila ya wanazi"hata mwenyekiti wa baraza kuu la waislam wa Ujerumani Aiman Mazyek anaunga mkono maandamano ya aina hiyo.

Wabunge watatu wenye asili ya kituruki wametoa mwito wa pamoja wa maandamano.Sevim Dagdelen wa kutoka chama cha mrengo wa shoto Die Linke,Aydan Özoguz wa chama cha SPD na Memet kilic wa chama cha walainzi wa mazingira die Grüne wametoa mwito kuona wahamiaji wa´naoishi humu nchini bwakishiriki kwa wingi katika maandamano hayo.Kwa mabasi na tramu wangesafiri kutoka mji mkuu Berlin na miji mengine ya jimbo hilo kuelekea Dresden.Wahamiaji lakini hawashiriki sana katika maandamano-Kilic anahisi hali hiyo inatokana na kwamba sheria za uhamiaji kwa muda amrefu zilikuwa na vizuwizi na hivyo kukorofisha hamu yao ya kutaka kuwajibika kisiasa.

Wahamiaji wengi wanahiusi kana kwamba wanatumiwa tu kisiasa anasema Kilic.Inabidi iwekwe wazi lakini kwamba na sisi tuna mshikamano na jamii yetu na sheria msingi yetu" anasisitiza mwanasiasa huyo wa chama cha Die Grüne.

People light candles in front of the Frauenkirche (Church of Our Lady) in Dresden to protest against an Ultra-right activists march through the city centre to commemorate the 67th anniversary of the World War II bombing of the city, February 13, 2012. The destruction of Dresden, in which 25,000 people were killed and flattened the city, sparked a debate about whether breaking public morale through the raids was justifiable since the defeat of Hitler's Nazis was imminent by then. REUTERS/Petr Josek (GERMANY - Tags: ANNIVERSARY CONFLICT POLITICS)

Watu wawasha mishumaa mbele ya kanisa la Frauenkirche kuwakumbuka wahanga wa masha mbulio ya february 13 mwaka 1945

Mwito wa pamoja wa makanisa ya Kikristo

Katika maandamano dhidi ya siasa kali za mrengo wa kulia,maaskofu wa kiinjili na kikatoliki nao pia wametoa mwito wa pamoja.Kutokana na kishindo kilichosababishwa na kufichuliwa November mwaka 2011 mauwaji kadhaa yaliyofanywa na kundi la kigaidi linalojiita "Nationalsozialistischer Untergrund"-NSU-kundi la chini kwa chini la wanazi- maaskofu hao wamesema "ni muhimu mwaka huu kama watu wengi zaidi kutoka kila pembe wangejitokeza kutoa onyo bayana dhidi ya ugaidi wa mrwengo wa kulia na hisia za chuki dhidi ya binaadam".Lakini sio wawakilishi wote wa makanisa hayo wanaounga mkono mwito wa njia kufungwa.

Maandamano ya kuadhimisha siku Dresden ilipohujumiwa kwa mabomu,yatafuatiwa siku tano baadae,February 18 na mkutano wa hadhara ulioitishwa na ushirika wa wanasiasa,vyama vya wafanyakazi na makanisa.Kauli mbiu:"Moyo,hishma na ustahamilivu-Dresden imeamua inataka kupambana na wanazi mambo leo.Kama siku hiyo kweli itatokea-haijulikani.Maandamano waliyokuwa wafanye wafuasi wa siasa kali ya mremngo wa kulia yameakhirishwa.

Ndo kusema wanazi mambo leo wamesalim amri?

Wataalam wa usalama wanauangalia uamuzi huo wa kurudi nyuma kama ni ishara ya kujivuta na ukosefu wa msimamo wa pamoja ndani ya kundi hilo la wanazi mambo leo.Hayo yamejiri baada ya kujulikana kadhia ya mauwaji yaliyofanywa na wanazi mambo leo. Hali hiyo inawahusu pia wafuasi wa siasa kali za mrengo wa kulia NPD. Wawakilishi wa vyama vya kisiasa wanajadiliana kwa nguvu juu ya uwezekano wa kupigwa marufuku makundi hayo mawili yanayowakilishwa katika mabunge mawili ya majimbo.

Mwandishi:Fürstenau,Marcel/(DW,Berlin)/Hamidou Oummilkheir

Mhariri:Abdul-Rahman, Mohammed

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com