1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Michezo

FC Nüremberg

FC Nüremberg-mojawapo ya klabu mashuhuri za Bundesliga,ilitamba kuanzia 1920 hadi 1968.Msimu uliopita ilirudi kileleni ilipoizima Stuttgart,mabingwa kutotoroka na vikombe vyote 2 vya nyumbani.

default

I.FC Nüremberg ni klabu ya kusini mwa Ujerumani na mojawapo kati ya klabu 3 mashuhuri za mkoa wa Bavaria-Bayern Munich, mabingwa mara kadhaa,Münich 1860 na Nüremberg ambayo msimu uliopita ilitoroka na kombe la shirikisho la dimba la Ujerumani baada ya kuwalaza mabingwa –Stuttgart.

FC Nüremberg ni timu iliotamba sana kabla kuanzishwa kwa Bundesliga-Ligi ya sasa ya Ujerumani 1963:

Kati ya 1920 hadi 1968 ndio enzi ya Nüremberg iliponawiri.Kwani, katika kipindi hicho ilitwaa mara 9 taji la ubingwa la Ujerumani na mara 3 kombe la shirikisho la dimba la Ujerumani.

Baada ya kipindi hicho,Nüremberg,nyumbani mwa m akampuni ya Addis Das na Puma, ilibidi kungoja miaka 40 kutwaa taji jengine.

Na hii ilikua mwaka huu pale tarehe 26 mei katika uwanja wa olimpik wa Berlin hapo Mei 26,ilipowalaza mabingwa wa Ujerumani Stuttgart kwa mabao 3-2 na kuizuwia Stuttgart kuondoka na vikombe vyote 2-kombe la ubingwa na la shirikisho .

Kwa ushindi huo dhidi ya Stuttgart,mashabiki wa Nüremberg walihemkwa kana kwamba wameingiwa na wazimu.Aliekua baridi kabisa ni kocha wao-Hans Meyer ambae hivi sasa anaabudiwa kama mungu wa dimba.Meyer alisema,

„Nikijua kuwa mashabiki wa klabu hii, muda mrefu wakisononeka na kutoridika na mchezo wa timu yao,ushindi huu sasa ni jambo la kupendeza mno.“

Alisema Hans Meyer,kocha anaetoka mashariki mwa Ujerumani.

Ikiwa kwa kocha Hans Meyer, ushindi ule ni ‚jambo la kupendeza“ kwa rais wa FC Nüremberg Michael Roth ilikua kitu zaidi:

„Hatukuamini kuwa tungeshinda kombe la shirikisho la dimba la Ujerumani.Hii ni kwa kuwa klabu hii mnamo miaka mingi iliopita haikuwa ikifika mbali.“

Kila mara mashabiki wa Nüremberg hutupa macho miaka ya nyuma.Kwani, ukiwa ni shabiki wa Nüremberg, unabidi kumezea mambo mengi.Kilele cha machungu hayo kilikuja mwishoni mwa miaka ya 1960.

Kwanza tuzungumzie ushindi wa ubingwa wa 1968:

„Kituo cha gari-moshi cha mjini Nüremberg kilikua shina la mashabiki waliokuwa wakishangiria.ukichukulia sherehe hasa za kuadhimisha ubingwa ziko njiani kufanyika,mwisho wa wiki inayokuja itakua asie na mwana aeleke jiwe na asie na mguu atie gongo.“

Kocha wa enzi zile Max Merkel aliamua kuwatunza wachezzaji vitita vya fedha kila mmoja kwa muujibu wa vile alivyocheza.

Merkel anakumbusha:

„Namna tulivyotwaa ubingwa wakati ule ,itakuwa vigumu kufanya hivyo tena.Kwa fedha tulizotoa ,kuna wachezaji waliotaka kuhamia Nüremberg na kuna wengine waliotaka kuihama Nüremberg kwenda Berlin.Mwishoe,wote walikimbia.“

Kocha Max Merkel msimu uliofuatia alibidi kucheza na timu mpya kabisa.Alibidi kuajiri wachezaji 13 wapya.Na hivyo kazi ya kuteremka mlima kwa Nüremberg ikaanza:

Kwani, kutoka mwaka wa kutwaa ubingwa ukafuata mwaka wa kuteremshwa daraja ya kwanza kwenda ya pili.Huu ni mkasa ambao haukuwahi kutiokea katika historia ya Bundesliga.

Miaka 9 iliofuatia 1968,GFC Nüremberg ikahamia ghorofa ya chini ya Ligi ya ujerumani.1999 ikarudi daraja ya kwanza.

Mnamo miaka ya 1980 Rais wa Nüremberg,Michael

Roth alikuja na mkakati mpya ambao hata Halmashauri kuu ya klabu hii haijakuwa tayari kuukubali kwa urahisi.Ilihisi anakwenda mbali mno.

Alilenga shabaha kileleni na sio kushinda kombe la shirikisho tu na kumaliza msimu nafasi ya 6.Alijenga timu upya na Nüremberg ikaanza kutamba tena.Haukupita muda lakini ikatwaa msimu uliopita Kombe la shirikisho na nafasi nzuri katika ngazi ya Bundesliga.

Leo, timu yoyote inayocheza na FC Nüremberg, inajiwinda barabara.Kwani, madume wa miaka ya 1920-1968 wamerudi kutamba.

 • Tarehe 17.07.2007
 • Mwandishi Ramadhan Ali
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/CHbg
 • Tarehe 17.07.2007
 • Mwandishi Ramadhan Ali
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/CHbg