1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

FC Kolon na Hamburg zachungulia daraja la pili

Sekione Kitojo
5 Machi 2018

Mabingwa  watarajiwa  Bayern Munich hawashikiki , waisambaratisha Freiburg , Kolon  na Hamburg  zachungulia  daraja la  pili.

https://p.dw.com/p/2tjOg
Fußball | Bundesliga 25.Spieltag | 1. FC Köln - VfB Stuttgart
Mlinda mlango wa FC Kolon Timo Horn akiwa amekaa chini baada ya kushindwa katika mchezo dhidi ya VFB StuttgartPicha: picture-alliance/Pressefoto Rudel

Kwa  upande  wa  Ligi  ya  Ujerumani  Bundesliga , mabingwa watetezi na  watarajiwa  Bayern Munich walishinda  jana  kwa mabao 4-0  dhidi  ya  Freiburg  na Bayern  inayofukuzia ubingwa wa sita mfululizo , imefungua  mwanya  wa  pointi 20  dhidi  ya  timu iliyoko  nafasi  ya  pili  Schalke 04 ikiwa  imesalia  michezo 9 ligi kumalizika. wiki  hii  hata  hivyo  timu zilizonufaika  katika  mchezo wa  25 ni  pamoja  na  Schalke 04 ,  iliyoishinda Hertha  Berlin  kwa bao 1-0  na  kuchupa  hadi  nafasi  ya  pili  katika  msimamo  wa  ligi.

Fußball | Bundesliga 25.Spieltag | RB Leipzig - Borussia Dortmund
Wachezaji wa Dortmund wakiokota mpira kutoka katika nyavu za RB LeipzigPicha: Reuters/A. Schmidt

Borussia  Dortmund  iliambulia  sare  ya  bao 1-1  dhidi  ya  RB Leipzig na  kuenguliwa  kutoka  nafasi  ya  pili  hadi  ya  tatu, wakati RB Leipzig ilibakia  katika  nafasi  ya  6.

Heka heka  hata  hivyo  ilikuw  katika  nafasi  ya  kuwnia  kujinasua kutoka mkiani  kwa  timu  mbili  kongwe, Hamburg SV  na FC Kolon ambazo  kabla  ya  kuingia  katika  mchezo  wa  25 zilikuwa zinafungana  kwa  poinzi , zote  zikiwa  na  pointi 17. Hamburg SV iliikaribisha  Mainz 05   katika  pambano  la  timu zinazowania kujinasua  kutoka  mkiani  ambapo pambano  hilo  lilimalizika kwa sare  ya  bila  kufungana. Matokeo  hayo  hayakuisaidia  sana Hamburg  ambayo  imefikisha  sasa  pointi 18.

Mkurugenzi  wa sporti  wa  Hamburg SV Jens Todt  baada  ya mchezo  huo  alikuwa  na  haya  ya  kusema.

Fußball Bundesliga HSV - Mainz 05
Pambano kati ya HSV dhidi ya Mainz 05 lilimalizika kwa sare ya bila kufunganaPicha: picture-alliance/dpa/A. Heimken

"Ni jambo  la  kusikitisha  kwamba  hatukuweza  kushinda  mchezo ule. Licha  ya  mbinyo  mkali  na  kuudhibiti  mchezo, kwa  muda  wa dakika  30 na  licha  ya  nafasi  kadhaa  tulizopata.  Nafasi zilikuwapo,  za  kushinda. Tulipaswa  kushinda, na  uwezekano ulikuwapo kama  nilivyosema. Hatukuweza tu  kufunga  bao, na mfanyaiko  ni  mkubwa."

FC Kolon

Mshambuliaji  raia  wa  Peru Claudio Pizarro  amekuwa  mchezaji  wa nne  mwenye  umri  mkubwa  kufunga  bao  katika  Bundesliga wakati  FC Kolon ilipopata  bao  la  kuongoza  nyumbani  dhidi  ya VFB Stuttgart  kabla  ya  mchezaji  wa  timu  ya   taifa  ya  Ujerumani Mario Gomez  kujibu kwa  kufunga  mabao 2 na  kuipa  ushindi  timu yake  wa  mabao 3-2 ugenini.

1. FC Köln - VfB Stuttgart Horn
mlinda mlango wa FC Kolon Timo Horn akisikitika baada ya timu yake kushindwa kupata pointi dhidi ya StuttgartPicha: picture-alliance/dpa/R. Vennenbernd

Pizarro mwenye  umri  wa  miaka  39, aliipatia  bao FC Kolon  iliyoko mkiani  kabisa  kwa  msimamo  wa  ligi  bao  katika  dakika  ya  saba na  sasa  amepachika  wavuni  takriban  bao  moja  katika  kila mchezo  wa   Bundesliga  katika  muda  wa  miaka  20. Lakini  data hizo  hazikuisaidia klabu  hiyo  kupata  matumaini  ya  kubakia  katika ligi  daraja  la  kwanza  kwani bado  imesalia  kuwa  timu  ya  mwisho miongoni  mwa  timu  18  za  Bundesliga. Huyu  hapa  kocha  wa timu  hiyo  Stefan Ruthenbeck.

"Katika  muda  wa  dakika  44  tlicheza  kandanda  safi  kabisa, tulipaswa  kuongoza kwa  mabao  2-0  ama  3-0. Kwa makosa ya mchezaji , ambayo  hayapaswi  kutokea tena , tuliteleza  na  kuwa nyuma. Tulizinduka  tena  mwanzoni  mwa  kipindi cha  pili  na  kisha tukarudi  tena  nyuma. Nafikiri  pia tungetumia   nafasi  tulizopata tungekuwa  mbele bila  shaka, kutokana  na nafasi  za  wazi tulizozipata. Kwa  hiyo inaumiza, lakini  hakuna  sababu  ya  kulalmika tu. Tunapaswa  kuangalia  mbele  na  tuone , iwapo dhidi  ya Bremen tunaweza  kupata  kitu."

Mwandishi: Sekione  Kitojo /  dpae / rtre / afpe
Mhariri: Yusuf Saumu