1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

FC Kaiserslauten

Ramadhan Ali31 Julai 2007

FC Kaiserslauten ndio timu ya bundesliga iliozusha maajabu 1996.Ilitoka daraja ya pili chini ya kocha Otto Rehagel na kupanda daraja ya kwanza.Msimu huo huo ikatawazwa mabingwa wa Ujerumani.

https://p.dw.com/p/CHbV

FC Kaiserslauten imekuwa ikiandika historia yake tangu miongo kadhaa katika Ligi ya Ujerumani kabla na baada ya Bundesliga kuasisiwa.

Hii ni timu yenye maskani yake kwenye bonde la Betzenberg na kupanda mlima huo timu yoyote nje ya Kaiserslauten hubidi kujiwinda barabara.

“ROTEN TEUFEL” au mashetani wekundu ndilo jina la timu hii na ni mashetani wa kugopwa.Kwani ni klabu gani inayothubutu kutoka daraja ya pili kuja ya kwanza na kutoroka na ubingwa.

Klabu nyingi hupepesuka na hupigana tu zisirudi daraja ya pili zilikotoka.Kwa Kaiserslauten,wao walitaka makubwa zaidi 1996.

Ilipoteremshwa daraja ya pili msimu wa mwaka juzi na ikijaribu msimu uliopita kurudi tena daraja ya kwanza, shabiki wake mmmoja mpita njia alisema:

“Tangu mwanzo nilisema kwamba wataingiwa na hofu-yaani wangemaliza nafasi ya 4 katika ngazi ya Ligi.Lakini kuwa wameondokea nafasi ya 6,inanihakikishia ule wasi wasi wangu niliokuwa nao.”

Shabiki mwengine akasema yahuzunisha kuwa FC kaiserslauten sasa inacheza daraja ya pili ya Bundesliga.

Kucheza katika Ligi ya kwanza ilikuwa yafurahisha sana.Tukisafiri na timu kwenda katika viwanja vyengine kuiona inacheza.Lakini leo wachezaji wazuri hawapo tena wameiachamkono Kaiserslauten.

Hii ni klabu alioichezea kabla Miroslav Klose,mshambulizi wa taifa ambae sasa ametoka Werder Bremen msimu uliopita na amejiunga msimu ujao na Bayern Munich.

Uwanja mpya wa Kaiserslauten leo unaitwa kwa jina la nahodha wake wa zamani Fritz walter,yule nahodha wa timu ya Ujerumani ilioilaza Hungary na Puskas,1954 mjini Bern,Uswisi na kutawazwa mabingwa wa dunia.

Mafanikio yake makubwa barani Ulaya ni pale ilipocheza nusu-finali ya kombe la ulaya la UEFA 1982 na Real Madrid ya Spian ingawa ilikandikwa mabao 5:0.

1990 Kaiserslauten ikatwaa taji lake la kwanza kombe la shirikisho la dimba la Ujerumani.Halafu ikaja Juni, 1991 pale FC Kaiserslauten ilipotawauzwa kwa mara ya 3 mabingwa Ujerumani.

“sisi ni timu ya Walter” nahodha wao maarufu Fritz Walter.

Hapo tena jina la ‘mashetani wekundu’ “Roten Teufel” likazaliwa.

Akielezea ilikuaje FCK kupewa jina hilo nahodha na staid wake mkubwa Fritz walter alieleza:

“Hii ilitokana na jazi nyekundu za timu hii ambazo tukivaa msimu wa 1945/46……na wakati ule tukiwafurahisha mashabiki kwa staili yetu ya dimba la kushambulia.Hapo tena ghafula wakatuita “mashetani wekundu”.”

FC kaiserslauten ikaendelea kuseleleza mila yake hiyo ya mashetani wekundu na kutamba na hasa mnamo miaka ya 1950.FCK ilitamba hata kabla kuanzishwa kwa Bundesliga, 1963.Katika finali kwenye uwanja wa olimpik wa Berlin dhidi ya Preussen Munster,kaiserslauten ilitamba kwa mabao 2:1 na kutwaa taji.

Na hivi ndivyo ripota uwanjani alivyosimulia:

“Firimbi ya mwisho imelia na Kaiserslauten ni mabingwa wa Ujerumani.Kwa mabao 2_1 imeilaza Preussen Münster.”

1953 FCK ikajikuta tena finali na mara hii iliipiga kumbo Stuttgart kwa mabao 4:1 ili kutwaa tena ubingwa.

1954 ukawa mwaka wa Kombe la dunia nchini Uswisi na timu iliovuma barani Ulaya ilikua Hungary chini ya Puskas.Lakini, pale Ujerumani ilipokutana mara ya pili na Hungary katika finali, iliizaba mabao 3:2 mjini Bern:

O-Ton 11-Herbert Zimmermann,reporter

“mpira umekwisha.Ujerumani ni mabingwa wa dunia kwa kuilaza Hungary mabao 3-2.”

Miaka zaidi ya 53 baadae,1996 FCK ilitumbukia daraja ya pili na kuiokoa kuirejesha daraja ya kwanza ilikua kazi ya kocha mashuhuri wa Bundesliga na leo wa Ugiriki-Otto Rehagel:

Kwani ni yeye alieipandisha tena FCK daraja ya kwanza kutoka ya pili na msimu huo huo akaitawaza mabingwa wa Ujerumani.Rehagel akasema:

“Ningependa kuwashukuru watoto waliofanya mazowezi barabara na kucheza pia barabara.Pia shukurani kwa halmashauri kuu ya klabu hii ilionipa kila msaada na zaidi kabisa kwa mashabiki walioonesha imani kubwa kwa timu-asnate sana.”

FC Kaiserslauten, imerudi tena daraja ya pili na msimu mpya unaoanza August 13-wiki 2 kutoka sasa- itapania tena kurudi daraja ya kwanza.