1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Fainali ya kombe la DFB kwa soka la wanawake Ujerumani

25 Machi 2011

Fainali ya soka la wanawake kuwania kombe la shirikisho la soka la Ujerumani DFB inafanyika Jumamosi hii mjini Cologne kati ya Turbine Potsdam na FFC Frankfurt.

https://p.dw.com/p/10hRM
Mabingwa wa ligi ya soka ya wanawake ya Ujerumani Bundesliga FFC Turbine PotsdamPicha: dapd

Mpaka siku ya Alhamisi tiketi elfu 17 kwa ajili fainali hiyo zilikuwa zimekwishanunuliwa. Turbine Potsdam wanajiwinda kushinda kombe la pili baada ya wiki iliyopita kutwaa ubingwa wa bundesliga, katika fainali iliyoudhuriwa na Rais wa Ujerumani Christian Wulff.

Meya wa jiji la Cologne Jürgen Roters amesema fainali hiyo itakuwa ni ya kusisimua na mwangaza wa soka la wanawake nchini Ujerumani kuelekea fainali za dunia za wanawake ambazo zitafanyika hapa Ujerumani mwezi wa sita mwaka huu.

Meneja wa FFC Frankfurt Siegfried Dietrich amesema fainali hiyo ni ndoto kwao.Naye kocha wao Sven Kahlert amesema msimu huu umekuwa wa kusisimua sana kwao.Amesema wameonesha kandanda zuri.

Mwandishi:Aboubakary Liongo/DPA

Mhariri:Othman Miraji