1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

EU yaishutumu Israel

28 Septemba 2010

Mkuu wa sera za nje wa Umoja wa Ulaya Catherine Ashton amesema hatua ya Israel kutorefusha muda wa usitishwaji wa ujenzi wa makaazi ya walowezi ni ya kusikitisha na ni kukiuka sheria za kimataifa

https://p.dw.com/p/POBV
Catherine AshtonPicha: AP
Nicolas Sarkozy Mahmoud Abbas Paris Treffen
Rais wa Mamlaka ya wapalestina Mahamoud Abbas kushito na Rais Nicolas Sarkozy wa Ufaransa kuliaPicha: AP

Rais wa Mamlaka ya Palestina Mahamoud Abbas hapo kabla alitishia kujitoa kwenye mazungumzo ya amani iwapo Israel ingechukua hatua hiyo.

Lakini amewaambia waandishi wa habari katika mkutano wake na Rais Nicolas Sarkozy mjini Paris, kuwa huenda akahirisha uamuzi wa kujitoa au kuendelea na mazungumzo na Israel, baada ya kukutana na wanadiplomasia wa nchi za kiarabu tarehe 4 mwezi ujayo.

Lakini msemaji wa Bwana Abbas,Nabil Abu Rudeina amesisitiza umuhimu wa kusitishwa kwa ujenzi wa makaazi hayo.

Kwa upande wake Rais Sarkozy amesema atawaalika mjini Paris kwa mazungumzo ya amani Rais Abbas, Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na Rais Hosni Mubark wa Misri.

Mwandishi:Aboubakary Liongo

Mhariri:Josephat Charo