1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

EU yaidhinisha jeshi la amani la Darfur

29 Januari 2008
https://p.dw.com/p/CzMC

BRUSSELS

Mawaziri wa mashauri ya kigeni wa nchi za Umoja wa Ulaya katika mkutano wao mjini Brussels wamekubali kutumwa kwa kikosi cha kulinda amani katika nchi za Chad na Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Lengo ni kuwalinda wakimbizi pamoja na wafanya kazi za misaada dhidi ya ghasia katika mkoa wa Darfur wa nchi jirani ya Sudan.

Hata hivyo,mkuu wa jeshi la Umoja wa mataifa la kulinda amani –Jean Marie Guehenno amesema kuwa kikosi hicho huenda kikacheleweshwa kukamilishwa.

Wanajeshi wanaohitajika wanafikia 3,700 na wamepangiwa kutumwa huko mda wa wiki chache zijazo.