Katika kipindi hiki tunazungumzia meno. Meno ya Jack yanamuuma sana. Tutafahamu pia ni mnyama yupi mwenye meno makali kuliko wote.
Abiy Ahmed aliyeteuliwa mwezi uliopita na muungano unaotawala nchini Ethiopia na Aprili 2 kuapishwa kuwa waziri mkuu ametangaza uteuzi wa baraza hilo katika televisheni ya taifa
Rais Raul Castro wa Cuba anastaafu na kukabidhi madaraka kwa makamu na mtu wake wa karibu, Miguel Diaz-Canel, lakini wengi wanaona mabadiliko haya hayana maana ya kubadilisha mfumo wa kisiasa na kiuchumi.
Israel imeanza maadhimisho ya kutimiza miaka 70 tangu kuundwa kwake ambapo waziri mkuu wa taifa hilo Benjamin Netanyahu ametumia maadhimisho hayo kuwaonya maadui zake na kugusia mahusiano na baadhi ya mataifa ya kiarabu.
Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com