EL-FASHER : Waasi wa Dafur wasusia mazungumzo | Habari za Ulimwengu | DW | 27.10.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

EL-FASHER : Waasi wa Dafur wasusia mazungumzo

Makundi mawili makuu ya waasi wa Dafur yamesema yatasusia mazungumzo ya amani yaliopangwa kuanza leo hii katika mji mkuu wa Libya Tripoli.

Kwa mujibu wa habari kutoka El-Fasher nchini Sudan hatua hiyo ni pigo kubwa kwa mazungumzo hayo ambayo Umoja wa Mataifa ilikuwa ikitumai kwamba yatapelekea kufikiwa makubaliano ya kudumu kwa jimbo hilo la Dafur lililoathiriwa na vita magharibi mwa Sudan.

Makundi hayo yanayosusia mazungumzo hayo ya amani ni ya Vuguvugu la Haki na Usawa na SLA-Unity ambalo linatuhumiwa kuhusika na mauaji ya wanajeshi 10 wa kulinda amani wa Umoja wa Afrika huko Dafur mwezi uliopita.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com