1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Dynamo Dresden

15 Juni 2007

Dynamo Dresden leo ikicheza daraja ya 3 ya Ligi ya Ujerumani,ikitamba zamani katika ile iliokua Ujerumani Mashariki.ilibuka mabingwa mara 8 na alao mara moja ilitamba katika kombe la Ulaya ilipocheza na Glasgow Rangers huko Scotland.

https://p.dw.com/p/CHby

Katika mlolongo wetu wa kuwajulisha klabu za Ligi ya Ujerumani-Bundesliga-leo ni zamu ya Dynamo Dresden-klabu ya Ujerumani mashariki ambayo baada ya kutamba na kuibuka mabingwa mara 8 katika iliokua Ujerumani mashariki leo imezama daraja ya tatu.

1967, Dynamo Dresden itakumbukwa, ilicheza kwa mara ya kwanza katika kombe la Ulaya.

Mjini Glasgow,Dresden ilikumbana na Glasgow Rangers.Timu ikaitumia fursa hiyo ya kucheza huko Scotland kwa kwenda cinema.Dieter Riedel ,enzi zile alikuwa mshambulizi kijana-shabab,leo ni mwalimu wa michezo huko kwao Dresden.Hawezi kuusahau mpambano ule katika uwanja wa Ibrox-Park,lakini pia ziara yao katika cinema.

Anasema:

“Ndio ,hebu nikumbushe haraka ,ilikua filamu gani.Ah,ilikua ya James Bond,barabara.Kwani ,ilieleza binadamu hufariki mara 2.”

Kwa kweli, Dynamo Dresden imefariki zaidi ya mara mbili na kufufuka.Katika ile iliokua GDR-Ujerumani mashariki,Dynamo Dresden imeibuka mabingwa mara 8 na imetia kikapuni mwake kombe la shirikisho la dimba la huko mara 7.Lakini pia, Dynamo Dresden ilijionea misukosuko ya kuteremshwa daraja ya pili kwa lazima ,kuwa na mashabiki wenye siasa kali pamoja na kuwa na rais –mjenzi wa majumba aliwaahidi fedha nyingi na baadae kukaribia kuifilisi klabu hii.

Leo hii Dynamo DFresden, imeangukia Ligi ya kimkoa au ya daraja ya tatu n a mashabiki wake wanayumbayumba kati ya hisia za hasira kwa hali ilivyo leo na za ukumbusho mwema wa enzi zao za kale Dresden ilipotamba katika ile iliok,ua Ujerumani mashariki kwa kutwaa ubingwa hadi mara 8.

Enzi zake za kukumbwa Dynamo Dresden,zilianzia 1969 pale kocha wake Walter Fritzsch, aliposhika usukani wa timu hii.1971 Dynamo kwa mara ya kwanza ilitwaa vikombe vyote viwili huko GDR-Ujerumani mashariki-taji la ubingwa na kombe la chama cha mpira cha huko.1973 nusra waitie munda Bayern Munich na kuiangusha katika kombe la Ulaya.Baada ya duru ya kwanza ya mabao 3:3,Munich ilitoroka mwishoe, na ushindi wa mabao 4:3 .hata Dieter Riedel alikuwa uwanjani katika changamoto hii ya awali kabisa kati ya timu 2 za nchi 2 za Ujerumani-mashariki na magharibi enzi zile.Riedel anakumbusha:

“Wakati ule haikuwa Bayern Munich yah ii leo yenye kutamba.Kwani,ilizabwa mabao 7:3 na kaiserslauten katika Ligi.Kwa kweli,ilikua timu unayoweza kuishinda.Lakini walitufunza darasa.”

Asema Riedel.

Mnamo miaka ya 1980,Dynamo Dreseden ilipata mpinzani mkubwa-yaani Dynamo Berlin.Ikisaidiwa na STASI –Idara ya Usalama ya iliokua Ujerumani mashariki- Dynamo Berlin iliibuka mabingwa mara kadhaa na kuigubika Dynamo Dresden.

Kwani, mkuu wa idara hiyo ya usalama Erich Mielke, akimpa muongozo moja kwa moja rifu vipi kupiga kipenga chake Dynamo Berlin inapoingia uwanjani.Juu ya hivyo, Dynamo Dresden iliibuka mara 3 mshindi wa kombe la shirikisho la dimba Ujerumani mashariki na kuilaza Dynamo Berlin.

Kulikuwapo mpambano mwengine kati ya timu 2 za Ujerumani mbili:Baada ya ushindi wa mabao 2:0 ugenini,Dynamo Dresden ikiongoza kipindi cha mapumziko tayari kwa mabao 3:1 hapo 1987 dhidi ya timu ya Ujerumani magharibi-Bayer Uerdingen.Lakini,Uerdingen ilidai kutangulia si kufika.

Mtangazaji dimba wa radio ya GDR-Ujerumani Mashariki aliefadhahika alisikika hivi:

"Lippmann kaukosoa mpira.Mara kwa mara mchezaji mwengine wa Uerdingen akitia fora usoni.Halafu, ikaja pasi na kwa fikra zangu Schäfer alikua ameotea,lakini kwa kweli hakuotea…akautandika mkwaju na ukaingia-bao.Jaribio la kuokoa alilofanya Dorner,lilikuwa bure.”

Hadi 1995,Dynamo Dresden ikicheza daraja ya kwanza ya Bubndesliga kufuatia muungano 1990. Ilikua enzi ya Dynamo kuwa na rais Rolf-Jürgen Otto,mepari mkubwa wa kampuni la ujenzi.Alipoisukuma Dresden ukingoni mwa kufilisika, Drsden ,ililazimishwa kuteremshwa daraja ya 3 ya Bundesliga.Baada ya pigo hilo,Dynamo Dresden ikatoweka muda mrefu kutoka medani ya dimba la malipo-pro-football.

Na ikoje hali ya Dynamo Dresden hii leo ?

Uwanja mpya wa dimba umepangwa kujedngwa kwa mashabiki hadi 32,000.Lakini mashabiki wa Dresden ni maarufu kwa fujo lao .

Sasa Dynamo Dresden imefufuka na imejiwinda kwa maisha ya pili-kwani matumaini ndio ya mwisho kufariki.