1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DUSHANBE.waandamanji wameapa kuendelea na shinikizo za kumtaka rais wa nchi hiyo ajiuzulu

3 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCwV

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Frank- Walter Steinmier amewasili nchini Tajikstan akiwa ziarani katika nchi za Asia ya kati.

Waziri Steinmier anatarajiwa kukutana na rais wa nchi hiyo Rahmonov katika mji mkuu wa Dushanbe.

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Frank-Walter Steinmier baadae ataelekea nchini Kirygystan ambako maelfu ya waandamanaji wameapa kuendelea na maandamano katika mji wa Bishkek leo hii kumlazimisha rais Kurmanbek Bakiyev ajiuzulu.

Maandamano hayo yalianza tangu jana wakati rais Bakiyev aliposhindwa kuwasilisha mabadiliko ya katiba ya nchi hiyo yenye kifungu kinacho mpunguzia uwezo katika mamlaka yake ya urais.