1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Dubai:Blair asema Iran ni kikwazo cha amani Mashariki ya kati.

20 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CChl

Waziri mkuu wa Uingereza Tony Blair ameishutumu Iran kwa kile alichokiita kuwa ni kikwazo kwa amani ya Mashariki ya kati na kuzitaka nchi zenye msimamo wa wastani katika eneo la Ghuba kuunda ushirika wa kupinga misimamo mikali. Akizungumza na wafanyabiashara wa Kiingereza katika mjini Dubai- Umoja wa Falme za Kiarabu- Bw Blair aliishambulia vikali Iran ambayo nchi za magharibi zinahofia inataka kuunda silaha ya kinuklea na kuishuku kuwa inayaunga mkono makundi ya wanaharakati kama Hezbollah nchini Lebanon na Hamas katika maeneo ya wapalestina. Blair yuko katika ziara ya nchi za Ghuba katika juhudi za kibalozi , kufufua mazungumzo ya amani ya Mashariki ya kati.