1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Man United kupambana na Brugge ya Ubelgiji

7 Agosti 2015

Manchester United wamepewa timu inayoonekana kuwa nyepesi katika droo ya mechi za mchujo za Ligi ya Mabingwa – Champions League, Club Brugge ya Ubelgiji.

https://p.dw.com/p/1GBnd
UEFA Champions League 2014-15 Auslosung
Picha: picture-alliance/dpa

Mabingwa hao wa zamani mara tatu, ambao wanarejea katika dimba la Ulaya baada ya kuwa nje kwa mwaka mmoja, watacheza mkondo wa kwanza uwanja wao wa nyumbani Old Trafford.

Katika droo nyingine, Wahispania Valencia, waliofika fainali ya mwaka wa 2000 na 2001, wamepangwa na Monacho ya Ufaransa wakati Lazio ya Italia ikishuka dimbani na Bayer Leverkusen ya Ujerumani iliyozabwa katika fainali ya 2002.

Sporting Lisbon itakuwa na nafasi ya kulipiza kisasi dhidi ya CSKA Moscow, waliowazaba katika Kombe la UEFA mwaka wa 2005 katika uwanja wa nyumbani wa Wareno hao mjini Lisbon.

Rapid Vienna ya Austria itachuana na Shakhtar Donetsk ya Ukraine wakati Celtic wakipangwa na Malmo.

Droo:

Astana (KAZ) v APOEL (CYP)

Skenderbeu (ALB) v Dinamo Zagreb (CRO)

Celtic (SCO) v Malmo (SWE)

Basel (SUI) v Maccabi Tel-Aviv (ISR)

BATE Borisov (BLR) v Partizan Belgrade (SRB)

Lazio (ITA) v Bayer Leverkusen (GER)

Manchester United (ENG) v Club Brugge (BEL)

Sporting Lisbon (POR) v CSKA Moscow (RUS)

Rapid Vienna (AUT) v Shakhtar Donetsk (UKR)

Valencia (ESP) v Monaco (FRA)

Michuano ya mkondo wa kwanza itachezwa Agosti 18 na 19 na ya marudio itakuwa Agosti 25 na 26. Washindi kumi watafuzu kazika droo ya hatua ya makundi yenye timu 32 mnamo Agosti 27 mjini Monaco.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA/Reuters
Mhariri: Iddi Sessanga