1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Drogba anakiongoza kikosi cha Cote d'Ivoire

9 Juni 2014

Didier Drogba anafahamu kuwa siku zake za kucheza katika Kombe la Dunia zinadidimia na kwamba dimba la Brazil 2014 huenda likawa fursa yake ya mwisho kuichezea Cote d'Ivoire.

https://p.dw.com/p/1CF49
Interaktiver WM-Check 2014 Mannschaft Elfenbeinküste
Picha: picture alliance/abaca

Drogba na wenzake mara nyingi hawajakuwa na bahati wakati wa kupangwa makundi katika vinyang'anyiro viwili walivyoshiriki. Katika mwaka wa 2006, walipangwa na Argentina, Uholanzi na Serbia na Montenegro katika duru ya kwanza. Na nchini Afrika Kusini, wapinzani wao katika awamu ya makundi walikuwa Brazil, Ureno na Korea Kaskazini.

Timu hiyo ya Mfaransa Sabri Lamouchi inataraji kuwa mara hii safari yao itamwendea vyema nahodha wao Didier Drogba mwenye umri wa miaka 33. Timu hiyo inajivunia majina ya kimataifa kama vile Yaya Toure, Salomon Kalou, Gervinho na wengine wengi. Licha ya ubora huo wa hali ya juu, hata safari yao ya kuelekea Brazil ilikuwa ngumu kuliko ilivyotarajiwa. Baada ya matatizo kidogo katika awamu ya makundi, Cote d'Ivoire karibu wabanduliwe nje kupitia mechi ya mchujo dhidi ya Senegal lakini Kalou akafunga katika dakika ya mwisho na kuwapa tikiti ya kuelekea Brazil.

Na mara hii The Elephants wamepangwa katika kundi C pamoja na Ugiriki, Japan na Colombia.

Mwandishi: Bruce Amani/dpa
Mhariri: Yusuf Saumu