DRESDEN:Putin aanza ziara nchini Ujermani leo | Habari za Ulimwengu | DW | 10.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

DRESDEN:Putin aanza ziara nchini Ujermani leo

Rais Vladmir Putin wa Urusi leo anatarajiwa kuwasili mjini Dresden kuanza ziara ya siku mbili nchini Ujerumani ambapo anatazamiwa kukabiliwa na maswali mengi juu ya kuuawa kwa mwandishi habari mashuhuri wa Urusi Anna Politkovskaya.

Bwana Putin atakutana na Kansela wa Ujerumani bibi Angela Merkel kwa ajili ya mazungumzo yatakayohusu pia suala la ugavi wa gesi na mafuta kutoka Urusi.

Kansela Merkel pia atazungumza na mgeni wake juu ya mauaji ya mwandishi huyo wa Urusi aliyekuwa mashuhuri kutokana na kuandika habari juu ya ukatili wa majeshi ya Urusi nchini Chechnya.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com