Dresden , Ujerumani. Mahakama yapingana na UNESCO. | Habari za Ulimwengu | DW | 07.06.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Dresden , Ujerumani. Mahakama yapingana na UNESCO.

Mahakama ya katiba nchini Ujerumani imetoa hukumu kuwa daraja linaweza kujengwa katika mto Elbe karibu na mji wa Dresden, licha ya vitisho vya shirika la umoja wa mataifa la sayansi , elimu na utamaduni UNESCO kuondoa hadhi ya urithi wa dunia kwa bonde la mto huo iwapo kazi hiyo ya ujenzi itafanyika.

Mahakama hiyo imetoa uamuzi huo kwa kukubali maoni miongoni mwa wakaazi wa mji huo wa mashariki ya Ujerumani ambao wamepiga kura kujengwa daraja hilo na kupunguza msongamano katika barabara za Dresden.

Mwaka uliopita , baada ya mkwamo wa aina hiyo, mji wa Kolon katika Ujerumani ya magharibi uliacha mipango ya kujenga majengo mawili marefu kutokana na jengo refu la kihistoria la kanisa kuu la mji huo baada ya shirika hilo la umoja wa mataifa kutishia kuondoa hadhi ya urithi kwa jengo la kanisa hilo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com