1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Dortmund dhidi ya Real, Bayern dhidi ya PSG

Bruce Amani
25 Agosti 2017

Droo ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya imefanyika mjini Nyon Uswisi ambapo kuna makundi kadhaa yenye mechi za kumezea mate. Ilikuwa siku ambayo pia Cristiano Ronaldo alitawazwa kuwa mfalme wa Ulaya

https://p.dw.com/p/2io0r
Schweiz Champions League Auslosung
Picha: picture alliance/dpa

Mabingwa watetezi Real Madrid watapambana na Borussia Dortmund na Tottenham Hotspur katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Mabingwa mara tano Barcelona wamepangwa na makamu bingwa wa msimu uliopita Juventus, pamoja na mabingwa wa Ugiriki Olympiakos na Sporting Lisbon.

Bayern Munich, watakuwa na kibarua dhidi ya Paris Saint Germain, pamoja na Celtic na Anderlecht. Timu nyingine pekee ya Ujerumani, RB Leipzig ambao wanacheza kwa mara yao ya kwanza katika Champions League, watachuana na Monaco, Porto na Besiktas ya Uturuki.

Wakati huo huo, mshambuliaji wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo ndiye mchezaji wa kwanza kushinda mara tatu tuzo ya UEFA ya mchezaji bora wa mwaka barani Ulaya. Mreno huyo alimpiku nyota wa Barcelona Lionel Messi na mlinda mlango wa Juventus Gianluigi Buffon. Katika upande wa wanawake, tuzo hiyo ilimwendea kiungo wa Barcelona, Mholanzi Lieke Martens

Orodha ya Droo kamili:

Kundi A: Benfica, Manchester United, Basel, CSKA Moscow

Kundi B: Bayern Munich, Paris St-Germain, Anderlecht, Celtic

Kundi C: Chelsea, Atletico Madrid, Roma, Qarabag

Kundi D: Juventus, Barcelona, Olympiakos, Sporting

Kundi E: Spartak Moscow, Sevilla, Liverpool, Maribor

Kundi F: Shakhtar Donetsk, Manchester City, Napoli, Feyenoord

Kundi G: Monaco, Porto, Besiktas, RB Leipzig

Kundi H: Real Madrid, Borussia Dortmund, Tottenham, Apoel

Mwandishi: Bruce Amani/AFP
Mhariri: Josephat Charo