1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Dick Cheney atoka hospitalini

27 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CTXf

Makamu wa rais wa Marekani, Dick Cheney, aliyegunduliwa na tatizo la moyo kutopiga kama kawaida, amepokea matibabu bila matatizo yoyote.

Madaktari katika hospitali ya George Washington wametumia kifaa cha umeme kuufanya moyo wake upige kama kawaida. Dick Cheney ameondoka kutoka hospitali ya George Washington na kurejea nyumbani kwake.

Anatarajiwa kuendelea na shughuli zake hii leo katika ikulu. Cheney mwenye umri wa miaka 66, ana historia ya matatizo ya moyo.

Madaktari walimpata na tatizo hilo la moyo hii leo wakati walipokuwa wakimtibu kikohozi kilichosababishwa na homa ya mafua.