1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Dhlakama atishia kushambulia

11 Aprili 2013

Kiongozi wa waasi wa Msumbiji Afonso Dhlakama ametishia kushambulia,vikosi vya serikali,ikiwa havitarejea nyuma kutoka kambi za mafichoni za RENAMO

https://p.dw.com/p/18E8V
Afonso Dlhkama,Mwenyekiti wa chama cha upinzani cha RENAMOPicha: Ismael Miquidade

Akiongea kutoka katika kambi yake iliopo kijijini katikati ya Msumbiji, Afanso Dhlakama, kiongozi wa zamani wa kundi la waasi wa Renamo,amekiri kuhusika na mashambulizi ya kituo cha polisi nchini humo kilichosababisha vifo vya askari wanne.

Amesema kuwa mashambulizi hayo yalikusudia kushambulia ofisi ya Renamo ambayo iliwatia mbaroni wafuasi 15 wa kundi hilo. ''Ninajua na mimi ndio niliyehalalisha, na kubariki mashambulizi hayo,'' amesema Dhlakama akiwataka wafuasi wake kuandaa mashambulizi mengine.

Mashambulizi hayo yanatajwa kuwa makubwa, kati ya viongozi hao wawili, ambao walisaini makubaliano ya amani ya Roma ya mwaka 1992 ambayo yalimaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumo kwa miaka15 nchini Msumbiji na kusababisha watu zaidi ya milioni moja kuuawa.

Vitisho vya nini

Mosambik Zusammenstöße RENAMO Rebellen mit Polizei
Wanamgambo wa RENAMO wakipatiwa mafunzo ya kijeshiPicha: Getty Images/AFP

Wachambuzi wa masuala ya kisiasa nchini humo, wanavitathmini vitisho vya kiongozi huyo wa waasi vya kurudi katika vita vya wenyewe kwa wenyewe, kuwa kama njia ya kujiinua kisiasa na kuonesha uwepo wa kiongozi huyo.

Mapema Novemba mwaka jana kiongoyi huyo wa waasi aliliambia shirika la habari la AFP kuwa alikuwa amepanga kuishambulia na kuiharibu Msumbiji iwapo eneo la Renamo halitapata sehemu za kubwa ya utajiri wa nchi hiyo.

"Ni bora kuwa na nchi masikini kuliko kuwa na watu tegemezi ambao wanaendelea kula katika mifuko yetu,' amesema kiongozi huyo wa waasi.

Njia muhimu za reli zinapita katika katika eneo hilo, zikichukua mafuta na gesi kutoka mkoa wa Moatize eneo la Tete sehemu ambayo mashirika ya uwekezaji ya Brazil na Australia yamewekeza kwa kiasi kikubwa.

"Ni kitu gani taifa letu linafaidika na jamii ya kimataifa katika uwekezaji wao hapa nchini, hata reli hii inayotumika kusafirisha mizigo hiyo kutoshambuliwa na vikosi vyetu," ameuliza Dhlakama kiongozi huyo wa waasi.

Nani wako nyuma ya mashambulio?

Mosambik Opfer von Zusammenstößen in Muxungue
Wahanga wa mashambulio ya MuxunguePicha: Fernando Veloso

Mbali na hilo lakini kiongozi huyo amepinga kuhusishwa na mashambulizi ya juma lililopita dhidi ya raia ambayo yalisababisha watu watatu kufariki na wengine kadhaa kujeruhiwa.

Kwa upande wake Rais wa nchi hiyo, Guebuza amelaani mashambulizi hayo na kusema kuwa serikali yake itaendelea kupigana ili raia wake waishi katika amani na utulivu, na bila kuishi na wasiwasi wowote.

Awali Rais Guebuza alimtaka kiongozi wa kundi la waasi nchini humo Dhlakama kufanya mazungumzo kuhusu hali ya kisiasa nchini humo, lakini kiongozi alifanya mkutano wa hadhara na kutoa masharti kwanza ya kuachiwa wafuasi wake 15 waliotiwa mbaroni.

Mwandishi: Hashim Gulana/AFP

Muhariri: Josephat Charo