DHAKA:Waziri mkuu wa zamani Khaleda Zia aachiliwa kwa dhamana
30 Septemba 2007Matangazo
Mahakama kuu ya Bangladesh imemuachilia kwa dhamana aliyekuwa waziri mkuu wan chi hiyo Khaleda Zia aliyekamatwa mapema mwezi huu kufuatia madai ya kuhusika katika ulaji rushwa.
Wakili wa Zia amesema mahakama imesimamisha vikao vya kusikiliza kesi juu ya rushwa dhidi ya Zia kwa mujibu wa sheria za dharura. Zia alikamatwa pamoja na mwanawe Arafat Rahman mnamo Septemba 3 kwa madai ya kutumia vibaya madaraka yake.Afisa wa mahakama hiyo amesema serikali inapanga kukata rufaa dhidi ya uamuzi wa kuachiwa kwa dhamana kwa Khaleda Zia.