1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DHAKA:Hali ya kutotoka nje yatangazwa

23 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBWf

Serikali ya Bangladesh inayoungwa mkono na jeshi imetangaza hali ya kutotoka nje kwa muda usiojulikana katika miji mikubwa sita huku huduma za simu za mkononi zikikatizwa kwa muda.

Amri hiyo imeanza baada ya vurugu za siku tatu za wanafunzi dhidi ya sheria ya hali ya hatari ilizoanza kutumika tangu mwezi Januari.

Mtu mmoja ameuwawa na watu wengine mia moja wamejeruhiwa kufuatia mapambano kati ya polisi na wanafunzi wanaotetea demokrasi nchini Bangladesh.