1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DHAKA: Rais wa serikali ya mpito ajiuzulu

12 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCbR

Rais Iajuddin Ahmed wa Bangladesh amejiuzulu waadhifa wake kama kiongozi wa serikali ya mpito. Kiongozi huyo pia ameahirisha uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika tarehe 22 mwezi huu nchini humo.

Akilihutubia taifa kwenye runinga, rais Ahmed alitanga pia hali ya tahadhari nchini Bangladesh. Uamuzi huu unafuatia mfululizo wa maandamano ya machafuko yaliyofanywa na wafuasi wa upinzani walikidai kwamba uchaguzi haungekuwa huru na wa haki.

Nafasi ya rais Ahmed itashikiliwa kwa muda na jaji wa mahakama kuu, Fazlul Haq, ambaye atakuwa na kibarua kigumu cha kuandaa uchaguzi mkuu. Kufikia sasa tarehe ya uchaguzi bado haijatangazwa.