1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

DHAKA: Maporomoko ya matope yameua watu 100 Bangladesh

Maafisa nchini Bangladesh wanasema,hadi watu 100 wamepoteza maisha yao katika maporomoko ya matope yaliotokea kusini-mashariki ya nchi kufuatia mvua mkubwa zilizonyesha.Matope hayo yamemiminika ndani na ukingoni mwa mji wa bandari wa Chittagong mapema siku ya Jumatatu.Ripoti zinasema,watu 10 wengine walifariki baada ya kupigwa na radi katika wilaya tatu mbali mbali zilizokumbwa na vimbunga.Vile vile si chini ya watu 15 wamepoteza maisha yao katika mvua na mafuriko yaliyotokea sehemu zingine za nchi. Imetabiriwa kuwa mvua zaidi zitanyesha nchini humo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com