1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Dhaka. Amri ya kutotembea ovyo yaondolewa kwa muda.

25 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBWE

Amri ya kutotembea ovyo katika miji sita nchini Bagladesh imeondolewa kwa muda jana na baadaye kurejeshwa , baada ya kudumu kwa muda wa siku tatu katika hatua ya kuimarisha madaraka ya serikali inayoungwa mkono na jeshi.

Amri hiyo iliwekwa siku ya Jumatano baada ya maandamano ya wanafunzi dhidi ya utawala wa kijeshi wa nchi hiyo kusambaa katika miji mingine ya nchi hiyo.

Amri ya kutotembea ovyo iliondolewa kwa muda siku ya Ijumaa na watu katika mji mkuu Dhaka jana walimiminika katika masoko kununua vyakula na mahitaji mengine na mitaa ilirejea kuwa tupu kabla ya amri hiyo kurejeshwa tena mchana.

Hapo mapema maprofesa watano wa chuo kikuu walikamatwa na majeshi ya usalama kwa madai kuwa walihusika katika maandamano hayo ambayo yalifikia katika hali mbaya siku ya Jumatano, na kusababisha serikali kutangaza amri hiyo ya kutotembea ovyo.