1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Darmstadt, Ujerumani. Mameneja wahukumiwa kifungo cha nje.

14 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC26

Mameneja wawili wa zamani katika kampuni kubwa la vyombo vya electroniki nchini Ujerumani la Siemens wamepewa hukumu ya kifungo cha nje kutokana na tuhuma za kutoa hongo.

Mahakama moja katika mji wa kusini wa Darmstadt imewapata watu hao na hatia ya kuhusika katika kutoa hongo kwa maafisa katika kampuni la nishati nchini Itali la Enel ili kupata mikataba minono ya kutengeneza mashine za kuzalisha umeme kwa kutumia gesi.

Hongo hiyo , yenye thamani ya Euro milioni sita , ilitolewa kati ya mwaka 1999 na 2002.

Mahakama hiyo imemhukumu meneja wa zamani Andreas Kley mwenye umri wa miaka 63 kifungo cha nje cha miaka miwili. Meneja mwingine mwenye umri wa miaka 73 Horst Vigener amepata kifungo cha nje cha miezi tisa. Kampuni hilo limeamriwa kulipa fidia ya kiasi cha Euro milioni 38.