1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DARGA, Ufilipino : Kimbunga chahofiwa kuuwa maelfu

4 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCmr

Wafanyakazi wa shughuli za uokozi wanasema idadi ya vifo kutokana na maporomoko ya ardhi yaliosababishwa na kimbunga cha mvua inaweza kuongezeka na kufikia maelfu.

Takwimu rasmi za serikali zinasema watu 425 wamekufa , 507 wamejeruhiwa na 599 hawajulikani walipo.Maelfu ya nyumba zimefukiwa na ziko chini ya vifusi vya volcano na matope vya futi tano.Waokozi wamekuwa wakitumia mikono na koleo kufukuwa maiti.

Rais Gloria Arroyo wa Ufilipino ametangaza hali ya maafa ya kitaifa na ametowa euro milioni 15 katika msaada wa dharura.

Kimbunga Durian ambacho kilipiga jimbo la Bicol nchini Ufilipino hapo Alhamisi kwa upepo uliokuwa uliokuwa na kasi ya kusafiri hadi kilomita 265 kwa saa na mvua mkubwa ni kimbunga cha nne kwa ukubwa kuikumba Ufilipino katika kipindi cha miezi minne.