1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DAMASCUS.Waziri mkuu wa Syria atazuru Irak

20 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCr2

Waziri mkuu wa Syria Walid al Moualem amesema kwamba nchi yake itaiunga mkono serikali ya Irak.

Waziri mkuu huyo anatarajiwa kuzuru Baghdad ambako atafanya mazungumzo na waziri mkuu wa Irak Nuri al Malik.

Ziara hiyo itakuwa ya kwanza tangu nchi hizo mbili zilipovunja uhusiano wao wa kidiplomasia na tangu kuondolewa madarakani aliyekuwa rais wa nchi hiyo Saddam Hussein mwaka 2003.

Alipoulizwa kuwa iwapo ziara hiyo ni kutokana na mwito wa waziri mkuu wa Uingereza Tony Blair ulioitaka Damascus kuingilia katim na kuisaidia Irak, waziri mkuu wa Syria Walid al Moualem amesisitiza kwamba ziara yake hiyo haiambatani na kuzifurahisha nchi za magharibi zenye nguvu.

Pia amesisitiza mwito wake juu ya kuondoka wanajeshi wa Marekani kutoka nchini Irak hatua ambayo anasema itapunguza mashambulio ya wapiganaji wenye msimamo mkali.