DAMASCUS:Syria yailalamikia Israel | Habari za Ulimwengu | DW | 06.09.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

DAMASCUS:Syria yailalamikia Israel

Syria imeilaumu Israel kwa kuingia katika anga yake na kufyatua mabomu na wakati huo huo imetishia kujibu mashambulio hayo.

Jeshi la Israel limesema halitatoa taarifa yoyote kuhusiana na madai hayo.

Hali ya wasiwasi imeongezeka kati ya nchi hizo mbili katika miezi ya hivi karibuni huku kukiwa na tetesi kutoka kwenye duru za upelelezi za Israel kwamba huenda utwala wa rais Bashar al Assad wa Syria ukajaribu kutwaa kwa nguvu baadhi ya maeneo ya milima ya Golan iliyotekwa na Israel katika vita vya mwaka 1967.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com