1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DAMASCUS:Syria ichangie kuleta utulivu Mashariki ya Kati

4 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCmf

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani,Frank-Walter Steinmeier anaikamilisha ziara yake ya siku nne katika Mashariki ya Kati kwa kukutana na rais Bashar al-Assad wa Syria mjini Damascus. Steinmeier,anataka kuishawishi Syria kutoingilia siasa za ndani za Lebanon na ichangie kuleta utulivu katika Mashariki ya Kati.Hata Marekani na Uingereza kimsingi zinaamini serikali ya Damascus yapaswa kushirikishwa zaidi katika juhudi za kuleta utulivu.Waziri Steinmeier siku ya Jumamosi alipokutana na waziri mkuu wa Lebanon Fouad Siniora,alitoa mito kwa majirani wa Lebanon kuheshimu uhuru wa nchi hiyo.