DAMASCUS: Syria na Irak kushirikiana kupambana na ugaidi
19 Desemba 2006Matangazo
Syria na Irak zimetangaza zitashirikiana katika vita dhidi ya ugaidi na uhalifu. Mawaziri wa mambo ya ndani wa nchi hizo mbili walisaini mkataba wa makubaliano hayo mjini Damascus hapo jana. Viongozi hao walisema wanataka kuunda mfumo mpya wa kuyalinda na kuyadhibiti maeneo ya mipaka yao.
Haya yametokea wakati Syria ikikosolewa kwa mara nyengine tena kwa kuwaruhusu wanamgambo wa kigeni kuingia Irak kupitia Syria.