1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DAMASCUS: Rais wa Irak aitembelea Syria

15 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCaR

Rais wa Irak Jalal Talabani yumo nchini Syria kujadili usalama na machafuko yanayoendelea nchini mwake pamoja na rais wa Syria Bashari al Assad. Syria imeahidi kufanya kila inaloweza kumaliza hali ya wasiwasi nchini Irak, siku chache baada ya Marekani kuilaumu Syria kwa kuchochea upinzani nchini Irak.

Rais Talabani, mwanasiasa wa Kikurdi aliyeishi uhamishoni nchini Syria kwa miaka kadhaa, ni rais wa kwanza wa Irak kuitembelea Syria katika kipindi cha karibu miongo mitatu. Ziara yake inalenga pia kuondoa uadui na kuboresha uhusiano kati ya Irak na Syria.