1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Damascus. Mkutano waahirishwa kati ya Abbas na kiongozi wa Hamas.

21 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCZH

Mkutano kati ya rais wa Palestina Mahmoud Abbas na kiongozi wa Hamas Khaled Meshaal umeahirishwa baada ya wasaidizi kushindwa kutatua tofauti juu ya kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa.

Mkutano huo ulipangwa kufanyika katika mji mkuu wa Syria Damascus jioni ya jana Jumamosi.

Mvutano wa kuwania madaraka kati ya chama cha Hamas na chama cha Abbas cha Fatah umepelekea kutokea ghasia katika eneo la Gaza na ukingo wa magharibi baada ya mazungumzo juu ya kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa kuvunjika mwishoni mwa mwaka jana. Hapo mapema , Abbas alikutana na rais wa Syria Bashar al-Assad, ambaye serikali yake imemruhusu kiongozi huyo wa Hamas anayeishi uhamishoni kuishi nchini Syria.