DAMASCUS: Habari za kutatanisha zatolewa kuhusu hatma ya mkutano kati Rais wa Palsetina na kiongozi wa chama cha Hamas, Khalid Mashaal | Habari za Ulimwengu | DW | 21.01.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

DAMASCUS: Habari za kutatanisha zatolewa kuhusu hatma ya mkutano kati Rais wa Palsetina na kiongozi wa chama cha Hamas, Khalid Mashaal

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon

Habari za kutatanisha zimetolewa kuhusu mkutano wa kujadili kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa uliopangwa kati ya Rais wa Palestina, Mahmoud Abbas, na kiongozi wa chama cha Hamas, Khalid Mashaal anayeishi uhamishoni mjini Damascus.

Afisa mkuu wa chama cha Hamas amesema mkutano huo, ulioahirishwa tangu jana, hautafanyika.

Hata hivyo, mpatanishi mkuu wa Palestina Saeb Ere amewaambia waandishi wa habari mkutano huo utakuwepo kiasi cha saa chache zijazo.

Rais Mahmoud Abbas amekuwa mjini Damascus kwa mashauriano na maafisa wa Syria.

Vyama vya Hamas na Fatah vimekuwa kwa muda wa miezi kadhaa vikijaribu kuunda serikali ya umoja wa kitaifa ili kuondolewa vikwazo vya ufadhili vilivyowekewa serikali ya Hamas na Umoja wa Ulaya pamoja na Marekani.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com