DAMASCUS: Chama cha Hamas chaikosoa Marekani | Habari za Ulimwengu | DW | 20.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

DAMASCUS: Chama cha Hamas chaikosoa Marekani

Naibu kiongozi wa chama cha Hamas, Moussa Abu Marzouk, ameikosoa vikali Marekani kwa kumbinya rais wa mamlaka ya Palestina, Mahmoud Abbas, ayakatae makubaliano ya kuunda serikali ya umoja wa taifa yaliyofikiwa baina ya chama cha Hamas na Fatah.

Marzouk aliuambia mkutano uliofanyika kwenye kambi ya wakimbizi ya Yarmouk kusini mwa Damascus nchini Syria kwamba sera ya Marekani imekita katika kupalilia uhasama miongoni mwa watu na mataifa ya eneo zima la Mashariki ya Kati.

Mkutano huo ulifanyika kupinga hatua ya Israel kuchimba kiwanja cha mahala patakatifu pa Haram al Sharif mjini Jerusalem.

Waziri wa mashauri ya kigeni wa Marekani Condoleezza Rice alisema mjini Ramallah Jumapili iliyopita kwamba Marekani itaamua kuhusu uhusiano wake na serikali mpya ya Palestina mara tu itakapoundwa.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com