1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Dalai Lama atoa mwito wa kuvumiliana miongoni mwa wafuasi wa dini

18 Mei 2008

-

https://p.dw.com/p/E23W

BERLIN

Kiongozi wa kidini katika jimbo la Tibet Dalai Lama ametoa mwito kuwepo na hali ya kuvumiliana miongoni mwa waumini wa dini zinazoongoza duniani.Akihutubia umati mkubwa katika mji wa Nuremberg kusini mwa Ujerumani leo hii Dalai Lama amesema dini imekuwa chanzo cha migogoro na umwagikaji damu katika miaka ya hivi kaeribuni.Kiongozi huyo wa kidini anayeihsi uhamishoni anakamilisha ziara yake nchini hapo kesho ambapo amepangiwa kuhutubia mkutano wa wanaharakati wanaunga mkono Jimbo la Tibet pamoja na kukutana na waziri wa misaada ya maendeleo Heidermarie Wizoerick Zeul.Kansela Angela Merkel hajaweza kukutana na kiongozi huyo kwasababu anafanya ziara Amerika ya kusini.Mwezi Septemba kansela Merkel alikutana na Dalai Lama na hali hiyo ilizusha mzozo mkubwa wakidiplomasia kati ya Ujerumani na China.