1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DAKAR : Wade ashinda uchaguzi wa rais

2 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCNP

Kiongozi mkongwe wa Senegal Abdoulaye Wade ameshinda kipindi cha pili cha urais katika uchaguzi uliofanyika hapo Jumapili na ameowaonya viongozi wa upinzani kwamba wanaweza kukabiliwa na uchunguzi wa rushwa uliositishwa wakati wa kampeni za uchaguzi huo.

Wade ambaye ameitawala nchi hiyo ya Afrika Magharibi tokea mwaka 2000 ameshinda karibu asilimia 56 ya kura na karibu mara nne zaidi ya mpinzani wake wa karibu.

Tume ya Taifa ya Kuhesabu Kura nchini Senegal imesema watu milioni 3. 4 wamepiga kura na Wade ameshinda kwa asilimia 55.9 wakati Waziri Mkuu wa zamani alieasiana na Wade Idrissa Seck ambaye aliwahi kufungwa kwa muda mfupi kwa madai ya rushwa hapo mkwa 2005 ameshika nafasi ya pili kwa kujipatia asilimia 14.9 na Ousmane Tanor Dieng wa chama kikuu cha upinzani cha Kisoshalisti ameshika nafasi ya tatu kwa kujipatia asilimia 13.6.

Wade alimtuhumu Seck kwa kushikilia mamilioni ya dola kwenye benki na kudokeza kwamba Tanor Dieng yumkini akawa amehusika na leseni za uvuvi zilizotolewa kwa njia ya rushwa chini ya serikali ya kishoshalisti iliopita.

Akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari katika

Jumba la Rais Wade ametahadharisha dhidi ya kumtafuta nani mchawi lakini amesema sheria lazima ichukuwe mkondo wake.