1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DAKAR : Habre kushtakiwa katika mahkama ya uhalifu

13 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBjM

Dikteta wa zamani wa Chad Hisene Habre ambaye anakabiliwa na mashtaka dhidi ya ubinaadamu atashtakiwa kwenye mahkama ya uhalifu na sio mahkama maalum kama ilivyokuwa imepangwa hapo awali.

Serikali imeeleza kwamba Rais wa Senegal Abdoulaye Wade amefikiria kutumia mahkama ya uhalifu iliofanyiwa marekebisho kuendesha kesi hiyo ya Habre anayeishi uhamishoni nchini Senegal kwa miaka 16.

Uchunguzi wa awali umeonyesha kwamba mahkama maalum ingeliweza kugharimu Afrika euro milioni 65.5.