1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

COPENHAGEN : Waandamanaji 300 mbaroni

17 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCii

Zaidi ya waandamanaji 300 wamekamatwa katika mji mkuu wa Danmark Copenhagen kufuatia mapambano ya kutumia nguvu na polisi.

Mapigano hayo yamezuka kutokana na mipango ya kufunga kituo cha vijana katika mji mkuu huo.Mzozo kuhusiana na kituo hicho cha vijana umekuwa ukitokota tokea mwaka 2000 wakati serikali ya mitaa ilipoliuza jengo lenye kituo hicho.

Wanaharakati wa sera za mrengo wa shoto wamekuwa wakikitumia kituo hicho kama makao yao makuu tokea mwaka 1982.

Mamia ya waandamanaji waliwavurumishia polisi mawe, chupa pamoja na fataki.Polisi walijibu mapigo kwa kuwashambulia waandamanaji hao kwa kutumia gesi ya kutowa machozi.