1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Congress ya Marekani kupasisha mpango wa Bush

Kalyango Siraj29 Septemba 2008

Mgogoro wa kifedha wasambaa Ulaya

https://p.dw.com/p/FQu7
Nancy Pelosi aonya kuwa huu ndio mwisho kuwadekeza wa Wall StreetPicha: AP

Watunga sera wa Marekani wamefikia mpango wa kuuyanasua mabenki kutoka katika mgogoro wa sasa wa kifedha.Wabunge hao wanatarajiwa kupiga kura kuunga mkono mpango huo wa donge la dola za kimarekani billion 700.Huku hayo yakiendelea mjini Washington mgogoro wa kifedha sasa umezikumba baadhi ya benki za Ulaya.

Wawekezaji duniani wanaikodolea macho Washington wakisubiri kitakachojiri kuhusu mgogoro wa kifedha.Hii ni kufuatia habari za kuwa wabunge wa pande zote yaani wa upande wa chama cha republican na wale wa Democratic kukubali kuupigia kura mpango wenye nia ya kuzinusuru benki zinazowakilishwa katika soko la hisa la Wall Street.

Hatua ya serikali ya kutaka kutumia pesa za walipa kodi zipatazo dola billioni 700 ili kuokoa wanaoweza kuiotwa mabwenyeye imezusha mvutano kati ya vyama hivyo viwili.Maafikiano haya mapya yamekuja baada ya malumbano ya siku tisa katika baraza la Congress.

Seneta Judd Gregg,mmoja wa wajumbe wa chama cha Republicans katika mazungumzo hayo katika kuupigia debe,ameuita mpango huo kama madhubuti.

Aidha amesema kuwa wabunge wa pande zote wamekubaliana kuhusu mpango huo ambao kwa maoni yake anaona kama utaleta uwiano kati ya madai ya Benki kuu ya Marekani huku kukiwa na usimamizi mkali wa walipa kodi.

Naye Spika wa baraza la wawakilishi la Marekani ambae anatoka katika chama cha democrat,Nancy Pelosi ameonya kuwa huo ndio mwisho wa kuwadekeza wasio jali katika soko la Wall Street.

Lakini baado kunaswali la ikiwa mpango huo wa Marekani ambao unatumia pesa za mlipa kodi kulipia deni la mikopo,kweli litarejesha imani katika masoko ambayo yanayumbayumba na pia kuondoa kuendelea kudidimia kwa uchumi.

Hii inatokana na kuwa mgogoro wa kifedha umesambaa kwingineko.

Katika ishsra kuwa mgogoro huo unaonekana umesambaa hata katika bara hili la Ulaya,serikali za Ubeligiji,Luxembourg na Uholanzi zimetaifisha shirika la fedhala Fortis.

Hii inatokana na mkutano wa dharura kati ya maafisa wa serikali husika pamoja na rais wa benki kuu ya Ulaya Jean-Calude Tricket kuhusu majaliwa ya shirika hilo ambalo ni miongoni mwa mashirika ya benki na bima 20 bora barani Ulaya.

Kwa mda huohuo shirika moja la kiingereza linatoa mikopo ya nyumba la Bradford & Bingley linakabiliwa na matatizo na huenda nalo likataifishwa.

Na hapa Ujerumani,shirika la nyumba la Hypo Real Estate limeomba msaada wa kifedha kutoka kwa benki kadhaa ili kuweza kuupiga jeki mtaji wake ambao unaonekana kama una mushkeli.