1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Condoleezza Rice kujadili migogoro ya Afrika

5 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CXQK

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Condoleezza Rice amewasili Addis Ababa nchini Ethiopia kujadiliana na wajumbe wa Umoja wa Afrika na wanasiasa kutoka maeneo ya migogoro ya bara Afrika.Kiini cha majadiliano hayo ni mapigano nchini Somalia,Sudan na mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.

Sudan imelaumiwa na Umoja wa Matifa kwa kutowalinda wakaazi wa jimbo la Darfur dhidi ya mashambulizi ya waasi,vikosi vya serikali na wanamgambo wanaoungwa mkono na serikali.Tangu mwaka 2003,zaidi ya watu 200,000 wameuawa katika jimbo la Darfur.