1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Condoleezza Rice akutana na Tzipi Livni mjini Washington

26 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CT3D

Waziri wa mashauri ya kigeni wa Marekani, Condoleezza Rice, amekutana na mwenzake wa Israel, Tzipi Livni, mjini Washington Marekani.

Mkutano kati ya viongozi hao ni sehemu ya juhudi za mwisho kuondoa tofauti zilizopo baina ya Israel na Palestina kabla mazungumzo kuhusu amani ya Mashariki ya Kati kuanza huko mjini Annapolis katika jimbo la Maryland.

Mazungumzo yao yametuwama juu ya waraka utakaowasilishwa kwenye mkutano.

Syria imethibitisha itahudhuria mkutano huo.

Waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert, amesema, ´´Rais wa mamlaka ya Palestina, Mahmoud Abbas, na waziri mkuu Fayyad, licha ya upinzani kutoka kwa Wapalestina wengi, wanataka amani na Waisraeli. Hii ni nafasi tunayotakiwa tuitumie.´´

Sambamba na hayo, maandamano ya amani ya kimadhehebu yaliyokuwa yafanyike mjini Annapolis yamefutiliwa mbali kutokana na ukosefu wa maafisa wa usalama kuwalinda waandamanaji.

Maandamano hayo yalipangwa kuanzia hekalu ya Beth Shalom hadi eneo la kumbukumbu ya vita vya pili vya dunia linalopakana na chuo cha mafunzo cha jeshi la maji la Marekani, ambako mkutano kuhusu amani ya Mashariki ya Kati unatarajiwa kuanza hapo kesho.