1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Condi awasili Kirkuk.

18 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CdAK

Baghdad.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Condoleeza Rice amewasili kaskazini mwa Iraq katika mji wa Kirkuk leo kwa ziara ambayo haikutangazwa kutokana na masuala ya kiusalama.

Alipowasili, waziri huyo alikuwa na mazungumzo ya faragha na maafisa wa eneo hilo na wawakilishi kutoka makundi ya kikabila, ikiwa ni pamoja na vyama vya kisiasa vya Wakurd na Waturuki.

Mji huo ambao unawakilisha jina la jimbo hilo, ni mji uliogawanyika kikabila na kuwa na mivutano wa muda mrefu baina ya Waarabu, Waturuki na Wakurdi, ambapo Wakurdi wanataka jimbo hilo lijumuishwe katika jimbo lenye mamlaka yake ya ndani la Wakurdi.

Bibi Rice anatarajiwa kukutana na viongozi wa Iraq mjini Baghdad baadaye leo. Kwa mujibu wa wa shirika la utangazaji la al-Arabia anatarajiwa kuwataka kuongeza juhudi zenye lengo la kufikiwa kwa maridhiano ya kitaifa.