1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

CONAKRY.Hali ya utulivu imerejea

15 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCS9

Hali ya utulivu imerudia katika mji mkuu wa Conakry nchini Guinea baada ya askari kupewa amri ya kupiga risasi na kuua.

Rais Lansana Conte alitangaza sheria za kijeshi dhidi ya waandamanaji na waporaji waliokuwa wanafanya vurugu mabarabarani.

Vurugu hizo zilitokea baada ya viongozi wa vyama vya wafanyakazi kuitisha mgomo kupinga uamuzi wa rais Conte wa kumchagua rafiki yake wa karibu Eugene Camara kuchukuwa wadhfa wa waziri mkuu.