1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

CONAKRY : Waandamanaji 23 wauwawa na 169 wajeruhiwa

23 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCYl

Polisi imewapiga risasi na kuwauwa waandamanaji 23 nchini kote Guinea hapo jana na kufanya idadi ya vifo kutokana na mgomo wa taifa wa takriban wiki mbili kufikia 33.

Watu 169 imeripotiwa kujeruhiwa nchini kote na 10 inasemekana wako mahtuti na wanaweza kupotea maisha yao wakati wowote ule kutokana na ukosefu wa vifaa na madawa ya matibabu.

Vyama vya wafanyakazi vimekuwa vikiongoza mgomo huo kushinikza kujiuzulu kwa Rais Lansana Conte ambaye amekuwa madarakani tokea mwaka 1984 baada ya mapinduzi yasiokuwa na umwagaji damu.Kiongozi hyuo mwenye umri wa miaka 72 anasumbuliwa na ugojwa wa kisukari na amewahi kulazwa hospitali mara mbili mwaka jana nchini Swirtzerland.

Kamishna wa Misaada ya Kibinaadamu wa Umoja wa Ulaya Louis Michel ametowa wito wa kuwepo kwa utulivu na kusema kwamba Umoja wa Ulaya unafuatilia kwa karibu hali hiyo nchini Guinea.