1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

CONAKRY : Rais Conte amtimuwa mshauri wake mkuu

20 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCZc
Waziri Mkuu Erdogan na mkewe Emine wakiusalimu umma uliokusanyika nje ya makao makuu ya chama cha AKP mjini Ankara,kusherehekea ushindi wa uchaguzi wa bunge
Waziri Mkuu Erdogan na mkewe Emine wakiusalimu umma uliokusanyika nje ya makao makuu ya chama cha AKP mjini Ankara,kusherehekea ushindi wa uchaguzi wa bungePicha: AP

Rais Lansana Conte wa Guinea amemtimuwa mshauri wake mkuu hapo jana katika kile kinachonekana kama jaribio la kutuliza mgomo mkuu lakini umoja wa vyama vya wafanyakazi katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi umesema hatua hiyo haitoshi kukomesha mgomo huo.

Conte amemuondowa Fode Bangoura waziri wa masuala ya urais na mtu mwenye nguvu kwenye kabila lake rais la Sousou na kumweka kwenye wadhifa huo Eugene Camara ambaye anaonekana kuwa ni mtu wa msimamo wa wastani katika serikali yake.

Viongozi wa vyama vya wafanyakazi wameitisha mgomo huo wa kazi ambao umeidumaza nchi hiyo kwa siku 10 mfululizo kwa sababu ya kile wanachosema kwamba Conte anayeuguwa ugonjwa wa sukari akiwa kwenye umri wa miaka ya 70 hafai kutawala na kwamba anapaswa kujiuzulu.

Takriban watu wanne wameuwawa wakati vikosi vya usalama vikipambana na waandamanaji nchini kote.