1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

COLOMBO:Waasi 15 wa Tamil Tiger wauwawa

23 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7DH

Wanajeshi wa Sri Lanka wamewauwa kiasi cha waasi 15 wa Tamil Tiger katika mapigano yaliyozuka kaskazini mwa nchi hiyo.

Duru za kijeshi zimesema wapiganaji wa Tamil Tiger walijaribu kuingia eneo linalosimamiwa na wanajeshi huko Vavuniya nje kidogo ya jimbo la linaloongozwa na waasi hao.

Hata hiyvo Viongozi wa Tamil Tiger wamekanusha taarifa za jeshi wakisema wapiganaji wake kadhaa wamejeruhiwa lakini hakuna aliyeuwawa.