COLOMBO.Mwanajeshi mmoja ameuwawa katika mapigano | Habari za Ulimwengu | DW | 29.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

COLOMBO.Mwanajeshi mmoja ameuwawa katika mapigano

Habari kutoka Sri Lanka zinaarifu juu ya kutokea mapigano kati ya majeshi ya serikali na waasi wa Tamil Tigers.

Taarifa za kijeshi zinasema kuwa mwanajeshi mmoja ameuwawa katika mapigano hayo katika eneo la mashariki mwa Sri Lanka.

Mapigano hayo yamezuka baada ya kiongozi wa waasi wa Tamil Tigers kusema kwamba makubaliano ya amani ya mwaka 2002 baina ya pande hizo mbili yamepitwa na wakati na kwamba kundi lake litaanzisha tena mashambulio ili kudai uhuru wa jimbo la Tamil.

Rais Mahinda Rajapakse wa Sri Lanka amehimiza kufanyike mazungumzo baina ya serikali na waasi ili kuepuka vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com